2026-08-05 Fundi Pro

Kwanini Taa ya Engine (Check Engine) Inawaka? Sababu 5 na Suluhisho

Feature
Taa ya check engine (Malfunction Indicator Light - MIL) ikiwaka kwenye dashboard yako, gari lako linakuambia kuwa kuna mfumo haufanyi kazi vizuri kupitia mfumo wake wa kitalaamu wa OBD-II (On-Board Diagnostics).

1. Sensor ya Oxygen (O2 Sensor): Hii hupima kiwango cha hewa chafu inayotoka kwenye moshi. Ikiharibika, gari hula mafuta mengi kuliko kawaida na inaweza kuharibu catalytic converter. Mara nyingi husababishwa na mafuta machafu au kukaa kwa muda mrefu bila kufanyiwa service.

2. Kifuniko cha Mafuta (Gas Cap): Hili ni tatizo dogo lakini la kawaida sana nchini Tanzania. Kifuniko kikilegea au kupasuka, hewa huingia kwenye tanki na kuvuruga presha ya mfumo wa mafuta (EVAP), jambo linalowasha taa ya engine mara moja.

3. Catalytic Converter: Hii husafisha moshi kabla haujatoka nje. Ikiziba (clogged), gari hupoteza nguvu na inashindwa kukimbia vizuri (stuttering). Hili ni tatizo la gharama kubwa, hivyo ni vyema kulikagua mapema.

4. Mass Airflow Sensor (MAF): Inapima kiwango cha hewa kinachoingia kwenye engine ili kompyuta ya gari iweze kujua kiasi sahihi cha mafuta kinachohitajika kwa ajili ya muunguko (combustion).

5. Spark Plugs & Ignition Coils: Plagi zikichoka, gari hutetemeka (misfiring) na kuwasha taa ya engine. Hii pia huongeza matumizi ya mafuta na kupunguza ufanisi wa engine.

SULUHISHO: Ili kujua tatizo la uhakika bila kubahatisha, unahitaji Diagnostic Scanner. Usibahatishe kwa kufuta kodi tu bila kurekebisha kosa! Pakua Fundi App sasa upate fundi mwenye scanner ya kitalaamu karibu nawe.

Video ya Maelezo

Unahitaji Fundi au Scanner ya Haraka?

Usiendelee kupoteza muda. Fundi App inakuunganisha na mafundi wenye vifaa vya kisasa karibu nawe popote ulipo Tanzania.

PAKUA FUNDI APP SASA

FREE DOWNLOAD • 8.8MB • APK