2026-08-05 Admin

Siri 5 za Kupunguza Matumizi ya Mafuta Kwenye Gari Lako

Feature
Kupunguza matumizi ya mafuta (Fuel Efficiency) hakuhitaji kubadilisha gari, bali kubadilisha tabia na kufanya matengenezo madogo ya kitalaamu:

1. Presha ya Matairi: Matairi yakiwa na upepo mchache, gari inakuwa nzito na engine inalazimika kutumia nguvu nyingi kusukuma gari, jambo linaloongeza matumizi ya mafuta.

2. Service ya Plagi na Filter: Filter ya hewa ikichafu, engine inatumia nguvu nyingi kuvuta hewa. Plagi zilizokwisha pia hupunguza kiwango cha mafuta yanayoungua vizuri (low efficiency).

3. Spidi ya Wastani: Kukimbia sana na kufunga breki ghafla (Aggressive driving) huongeza matumizi ya mafuta kwa karibu 30%. Endesha kwa kasi ya wastani na epuka dharura zisizo za lazima.

4. Punguza Mizigo: Mizigo mizito isiyo ya lazima kwenye buti huifanya gari iwe nzito. Kila kilo 50 za ziada zinaweza kuongeza matumizi ya mafuta kwa 1% mpaka 2%.

5. Tumia Mafuta ya Uhakika: Hakikisha unajaza mafuta kwenye vituo vinavyotambulika ili kuepuka mafuta yaliyochanganywa ambayo yanaweza kuharibu sensor na engine.

Fundi App inakuonyesha maduka ya spare bora kupata filter na plagi OG (Original) ili kuongeza ufanisi wa gari lako. Pakua app sasa kuanza kuokoa gharama za mafuta.

Video ya Maelezo

Unahitaji Fundi au Scanner ya Haraka?

Usiendelee kupoteza muda. Fundi App inakuunganisha na mafundi wenye vifaa vya kisasa karibu nawe popote ulipo Tanzania.

PAKUA FUNDI APP SASA

FREE DOWNLOAD • 8.8MB • APK