2026-08-11 Fundi Issa

Jinsi ya Kubadilisha Oili na Kichujio cha Oili

Feature
Utangulizi: Kubadilisha oili ni moja ya kazi muhimu zaidi za matengenezo unazoweza kufanya mwenyewe. Oili safi hupunguza msuguano na kuzuia injini kupata joto kali. Vifaa vinavyohitajika: Usalama: Hakikisha gari limepoa kabla ya kuanza. Usifanye kazi chini ya gari lililonyanyuliwa na jaki pekee; tumia stendi za usalama kila wakati. Hatua za kufuata:
1. Nyanyua gari kwa kutumia jaki na uweke stendi za usalama.
2. Tafuta nati ya kutolea oili (drain plug) chini ya injini na uweke chombo cha kukusanyia oili chini yake.
3. Fungua nati kwa kutumia spana na uruhusu oili yote itoke. Kuwa makini maana oili enaweza kuwa na joto.
4. Mara oili inapomalizika kutoka, rudishia nati na uifunge vizuri lakini usizidishe nguvu.
5. Tafuta kichujio cha oili na ukitue kwa kutumia spana ya kichujio. Paka oili kidogo kwenye mpira wa kichujio kipya na ufunge kwa mkono mpaka kishike vizuri.
6. Fungua mfuniko wa oili juu ya injini na umimine oili mpya kwa kiasi kinachopendekezwa na mtengenezaji.
7. Washa gari kwa dakika chache, kisha zima na ukague kiwango cha oili kwa kutumia kijiti cha kupimia (dipstick). Ongeza oili kama itahitajika. Hakikisha unatupa oili ya zamani katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kulinda mazingira. Hii ni hatua muhimu sana katika kuhakikisha injini yako inakaa kwa muda mrefu bila matatizo ya msuguano wa vyuma.

Unahitaji Fundi au Scanner ya Haraka?

Usiendelee kupoteza muda. Fundi App inakuunganisha na mafundi wenye vifaa vya kisasa karibu nawe popote ulipo Tanzania.

PAKUA FUNDI APP SASA

FREE DOWNLOAD • 8.8MB • APK